
Play all audios:
Alhamisi Kuu, tarehe 14 Aprili 2022, Papa Francisko ameadhimisha Ibada ya Misa kwenye Gereza la Civitavecchia “Casa Circondariale di Civitavecchia” nje kidogo ya mji wa Roma na kuhudhuriwa
na wafungwa, Askari pamoja viongozi wa Gereza. Hii ni Jumuiya kubwa inayoundwa na watu zaidi ya 900. Wafungwa ni 530 na wengi wao ni wanawake. Huduma ya huruma, upendo na msamaha. NA PADRE
RICHARD A. MJIGWA, C.PP.S. – VATICAN. Alhamisi Kuu Jioni: “Basi, kabla ya sikukuu ya Pasaka, Yesu, hali akijua ya kuwa saa yake imefika, atakayotoka katika ulimwengu kwenda kwa Baba, naye
aliwapenda watu wake katika ulimwengu, aliwapenda upeo”. Yn. 13:1. Haya ni maneno yanayofuatiwa na kitendo cha Kristo Yesu kuwatawadha wanafunzi wake miguu na kuifuta kwa kitambaa alichokuwa
amejifunga kiunoni. Katika Karamu ya Mwisho, “Coena Domini” Kristo Yesu, alijiandaa kujisadaka kwa mateso na kifo cha Msalaba. Maadhimisho ya Jioni ya Alhamisi Kuu yamesheheni matukio
mazito katika maisha na utume wa Kanisa. Hii ni siku ambayo Kristo Yesu alianzisha Sakramenti ya Ekaristi Takatifu, chanzo na kilele cha maisha na utume wa Kanisa. Alhamisi Kuu ni siku
ambayo Kristo Yesu alipoweka Sakramenti ya Daraja Takatifu ya Upadre, ili kufundisha, kuongoza na kuwatakatifuza watu wa mungu na hatimaye, akawapatia Amri mpya ya upendo inayomwilishwa
katika huduma makini kwa watu wa Mungu kama sehemu ya mchakato wa ujenzi wa upendo wa udugu wa kibinadamu na ufalme wa Mungu unaosimikwa katika: Ukweli, maisha, utakatifu, neema, haki,
upendo na amani. Papa Francisko amewaosha miguu wafungwa 12 wakiwemo wanawake watatu. NI KATIKA MUKTADHA WA MAADHIMISHO YA KARAMU YA MWISHO, ALHAMISI KUU, TAREHE 14 APRILI 2022, BABA
MTAKATIFU FRANCISKO AMEADHIMISHA IBADA YA MISA TAKATIFU KWENYE GEREZA LA CIVITAVECCHIA “CASA CIRCONDARIALE DI CIVITAVECCHIA” nje kidogo ya mji wa Roma na kuhudhuriwa na wafungwa, Askari
pamoja viongozi wa Gereza pamoja na Waziri wa Sheria nchini Italia Marta Cartabia. Hii ni Jumuiya kubwa inayoundwa na watu zaidi ya 900. Wafungwa ni 530 na wengi wao ni wanawake. Kati ya
waamini kumi na mbili waliooshwa miguu na Baba Mtakatifu Francisko walikuwemo wanawake watatu kutoka katika nchi mbalimbali. Baba Mtakatifu katika mahubiri yake amefafanua maana ya Kristo
Yesu kuwaosha miguu Mitume wake kuwa ni kielelezo cha upendo unaomwilishwa katika huduma makini na hivyo kukipatia maana mpya kwani hapo awali kitendo hiki kilitekelezwa na watumwa. Kristo
Yesu anawataka wafuasi wake wawe ni mfano wa huduma ya upendo kati yao. Wajitoe bila ya kujibakiza kwa ajili ya ustawi, maendeleo na mafao ya wengi. Ni huduma ambayo inapaswa kutolewa kwa
kuzingatia sheria, kanuni na taratibu za nchi na kamwe huduma hii isisimikwe kwenye rushwa na ubadhilifu wa mali ya umma. Waamini wajifunze kukimbilia na kuambata huruma na upendo wa Mungu
katika maisha. WAAMINI WAJIFUNZE KUKOSOANA KWA HURUMA NA UPENDO UNAOFUMBATWA KATIKA MSAMAHA WA KWELI UNAOBUBUJIKA KATIKA HURUMA NA UPENDO WA MUNGU ambaye kamwe hachoki kusamehe na kusahau.
Jambo la msingi ni kuhakikisha kwamba, wanakuwa na ujasiri wa kukimbilia huruma na upendo wa Mungu unaosimikwa kwenye Mahakama ya Huruma ya Mungu, yaani Sakramenti ya Upatanisho. Kristo Yesu
ni kielelezo cha ufunuo wa huruma na upendo wa Mungu kwa waja wake. Mwenyezi Mungu anasemehe yote na kamwe wasichoke kuomba huruma na msamaha wake wa daima. Mapadre wawe ni mfano wa kuigwa
katika huduma ya: Neno, Sakramenti za Kanisa na matendo ya huruma: kiroho na kimwili. Kamwe Mapadre wasitumie Daraja Takatifu kuwanyonya waamini wao, bali wawe ni vyombo na mashuhuda wa
huduma kwa watu wa Mungu; alama ya upendo na huruma ya Mungu kwa watu wote, bila ya kuwa na maamuzi mbele, bali daima wasukumwe na huduma. Kristo Yesu ndiye Hakimu mwenye haki, huruma,
upendo na msamaha. Maadhimisho ya Karamu ya Bwana, iwe ni Liturujia inayochochea Upendo unaomwilishwa katika huduma makini kwa watu wa Mungu na huruma na msamaha unaobubujika kutoka kwa
Kristo Yesu. Mara baada ya Misa Takatifu wafungwa wamemzawadia Baba Mtakatifu matunda ya kazi ya mikono yao, mwishoni, amewashukuru na kuwapatia wote baraka zake za kitume. Karamu ya Mwisho