Makamu wa rais wa iran aomba kujiuzulu

feature-image

Play all audios:

Loading...

Hayo yameripotiwa na Shirika la habari la Iran, IRNA ambalo limearifu kwamba Zarif, amewasilisha barua hiyo mapema leo kwa Rais Masoud Pezeshkian. Hiyo itakwua ni mara ya pili kwa Zarif


kutangaza kujiuzulu lakini hapo kabla haikufahamika iwapo Rais Pezeshkian alikubali ombi hilo. Mwanadiplomasia huyo aliyekuwa na dhima kubwa kwenye mkataba wa nyuklia  kati ya Iran na madola


yenye nguvu wa mwaka 2015 alipokuwa waziri wa mambo ya kigeni, amekuwa akilengwa kwa muda mrefu na wanasiasa ndani ya mfumo wa kidini unaoitwala Iran. Wanamlaumu kwa ushauri wake wa kila


wakati wa kutaka Terhan ijongeleane na Marekani na kumaliza tofauti zilizopo.